Tuesday, October 27, 2009

BREAKING NYUUUUUUZ!ITS BUSTER RHYIMS NDANI YA BONGO.

Habari zilizotufikia leo hii kutoka kwa Bwana Joseph Kusaga mkurugenzi wa Cloud Media ambayo ndiyo mmiliki wa redio ya Clouds F.M,Choice F.M,Clouds T.V na Primetime promotion ambao kwa ujumla ndiyo waandaaji wa tamasha maarufu la Fiesta ambalo zamani lilijulikana kwa jina la Summer Jam,safari hii wameamua kufanya kweli kwa kumleta mchizi ambaye ni mkali wa miondoko ya hiphop Buster Rhyimes pamoja na wazeiyya wake kama Flip n.k hii yote itakuwa ndani ya tamasha hilo ambalo kauli mbiu yake ya mwaka huu ni Fiesta One Love likisisitiza mshikamano kwa watanzania na litafanyika hapo tarehe 07.11.2009 kama kawa.Pamoja na hayo Bwana Kusaga ambaye pia anajulikana zaidi kwa jina la Jo ametoa shukrani za dhati kwa uongozi nwa serikali kwa mikoa yote ambayo tamasha hilo la Fiesta limeshafanyika kwa mwaka huu kwa kuanzia mkoani Dodoma mpaka wiki iliyopita lilipokuwa pale mjini Tanga,pia ametoa shukrani zake kwa wadhamini wote walioshiriki katika maandalizi yote ya Fiesta ya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment