Saturday, October 24, 2009

KESHO NI SIKU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

ASSALAAM ALAYKUM!
WADAU WATANZANIA WENZANGU NINA IMANI YA KUWA WENGI WENU MNAFAHAMU NA MMEJIANDIKISHA KWA AJILI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA VITONGOJI NCHI NZIMA.
KUMBUKA NAFASI HII NI MUHIMU KWA KUCHAGUA KIONGOZI BORA NA MWENYE KUWAJALI WANANCHI WAKE.
KIONGOZI BORA HACHAGULIWI KWA MBINU CHAFU ZA RUSHWA AU VIJIZAWADI BALI ANACHAGULIWA KWA MAZURI ALIYOYAFANYA AU ATAKAYOYAFANYA KWA WAKAZI WAKE HIVYO WATANZANIA WENZANGU MSIADAIKE NA WENYE KUJA NA MAHELIKOPTA AU VITENGE NA MALAND CRUISER YAO BALI TUMCHAGUE YULE TU AMBAYE ANAJALI NA TUPO NAE KWA KILA JAMBO.PIA TUJIEPUSHE NA VURUGU NA MARA TU BAADA YA KUMALIZA KUTUMBUKIZA KURA YAKO AMBAYO NI SIRI YAKO BASI MOJA KWA MOJA FUATA NJIA YA KUELEKEA NYUMBANI NA KUSUBIRI MATOKEO YA TAKAYOTANGAZWA NA VYOMBO HUSIKA.
NAWATAKIA KILA LA KHERI NA UCHAGUZI MWEMA.

No comments:

Post a Comment